MZUNGUKO wa 29 ulibaki na kicheko kwa timu ya Pamba jiji ilipokuwa mwenyeji wa JKT Tanzania mkoani Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba baada ya kuchomoza na ushindi ‘finyu’ wa bao 1-0 nyumbani.
Dakika ya 40 zilitosha kwa timu ya Pamba jiji kupata uongozi kwa bao lililofungwa na Zabona Mayombya.
Pamba jiji imejiweka nafasi ya 11 ikiwa na alama 33 huku JKT Tanzania ikisalia nafasi ya 6 na alama zake 35.
Katika mchezo huo mchezaji wa Pamba jiji Zabona Mayombya aliyefunga bao pekee alichaguliwa kuwa mchezaji bora na nyota wa mchezo huo.