RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amethibitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF kuwa Rais wa Shirikisho hilo kwa kipindi kingine cha miaka minne katika uchaguzi wa TFF uliofanyika jana Agosti 16 Mkoani Tanga.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo Rais Karia alisisitiza watu kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa changamoto mbalimbali zilizojitokeza huko nyuma.
“Nawashukuru leo mmenipitisha lakini twende tukafanye kazi, tuna hitaji taarifa kwenu na pia tutafatilia kwasababu tutakapofanya peke yetu huku juu chini hakufanyiki kitu hatuwezi kufanikiwa” alisema Rais Wallace Karia.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inampongeza Ndugu Wallace Karia na kumtakia kila la kheri kipindi kingine cha miaka minne ya majukumu yake.