NBC CHAMPIONSHIP KUPIGWA MIKOA SITA LEO.

 

LIGI ya NBC Championship mzunguko wa 20 unaanza leo Februari 3 kwa michezo sita kupigwa kwenye mikoa sita tofauti.

Mchezo wa mapema saa 8:00 mchana utazikutanisha Stand United dhidi Biashara United kwenye uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.

Mkoani Mbeya KenGold itaikaribisha Mbeya City saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Sokoine huku KenGold ikiingia kwenye mchezo huu ikiwa kinara kwenye msimamo na alama 43 kwenye michezo 19 huku Mbeya City ikiwa nafasi ya 7 na alama 32 kwenye michezo 19.

Mkoani Arusha ni “ Derby ya Jeshi” kati ya Mbuni na TMA saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid huku alama moja pekee ikiweka utofauti baina ya timu hizi TMA ikiwa nafasi ya nne na Alama 37 huku Mbuni ikiwa nafasi ya tano na alama 36 hivyo kuufanya mchezo huu kuwa wa kuvutia.

Mchezo mwengine utazikutanisha FGA Talents dhidi ya Polisi Tanzania saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Mkoani Mwanza Copco itaikabili Pamba kwenye uwanja wa Nyamagana saa 10:00 alasiri mchezo huu ukiwa ‘Mwanza Derby’ kutokana na timu zote kutokea mkoa wa Mwanza.

Mchezo wa mwisho utapigwa mkoani Pwani Pan African itaikabili Cosmopolitan kwenye uwanja wa Mabatini saa 10:00 alasiri.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *