LIGI Kuu ya NBC inatarajiwa kuendelea kesho kwa mchezo namba 148 ambapo timu ya Simba itaikaribisha timu ya Dodoma jiji katika uwanja wa KMC Complex mkoani Dar es Salaam majira ya saa kumi jioni.
Simba ipo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na alama 54 ikifunga mabao 46 na kuruhusu mabao 8 katika michezo 22 timu hiyo iliyocheza mpaka sasa.
Dodoma Jiji iko nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC huku ikiwa na alama 27 ikifunga mabao 22 na kuruhusu 27 katika michezo 22 iliyocheza mpaka sasa.
Mechi hiyo ya Simba na Dodoma Jiji iliahirishwa kutokana na ajali iliyopata timu ya Dodoma Jiji ikitokea Ruangwa mkoani Lindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya timu ya Namungo