KARIAKOO DERBY

KARIAKOO ‘DERBY’ KUPIGWA JUNI 25.

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeusogeza mbele mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC kati ya klabu ya Yanga na klabu ya Simba ambao ulipangwa kufanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Juni 15, 2025 kuanzia saa 11:00 jioni.

Mchezo huo sasa utafanyika Juni 25, 2025 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 11:00 jioni.

Bodi inazitakia maandalizi mema klabu za Yanga na Simba kuelekea mchezo huo.

8 comments

  1. Hongera kupata suluhu ya mchezo wa derby ya Kariakoo. Lakini kuweni makini kwenye maamuzi baada ya hii temporary solution. Mpira ni burudani kwa wengi.

  2. Bodi yetu Ligi mbona hamjasema sababu ya kusogeza mbele huo mchezo? Ni vyema muwe na sababu zinazoelezeka sio kutuoa taarifa ambayo inatuacha wapenzi wa Mpira tukiwa na Maswali Mengi yasiyo na majibu hivyo kubwabwaja na kutukanana Mitandaooni.

    Hali hii itasababisha wengi wetu tupoteze kabisa mapenzi yetu na Mpira wa Tanzania na kuamua kurudisha mapenzi na ushabiki wetu wa zamani katika Ligi za ulaya KISA, Mpira wetu kuwa na maamuzi yasiyoeleweka, mfano maamuzi ya Mchezo 184 kuanzia Machi 8.

    Mimi nilitegemea baada ya Simba kuandika barua yake Machi 7, Bodi ya Ligi ingejitokeza haraka sana asubuhi ya Machi 8 kwanza kukemea kitendo cha Simba kuzuiwa kufanya Mazoezi na Kisha kutoa ufafanuzi wa Kanuni na kuitaka Timu hiyo ikacheze huku taratibu za kuwapata waliowazuia zikiendelea ili kuwachukulia hatua husika. Kitendo cha kuhairisha Mchezo kilifanyika kimakosa. Lakini Bado mmeendelea kufanya Makosa ya Kupanga tarehe nyingine ya mchezo bila kutatua malalmiko ya timu zote mbili, Simba walitoa malalamiko ya maandishi ya kuzuiwa kufanya Mazoezi yaliyosababisha mechi kuharishwa na Yanga walitoa malamiko Yao kwa maandishi ya kuoridhishwa na kuhairishwa mchezo.

    Ushauri Wangu, tusaidiane kuomba tarehe 25/06/2025 mchezo huu uchezwe. Kinyume na hapo Taifa Letu litaingia kwenye Mgogoro wa Mpira wa Miguu unaoweza kasababisha athari kubwa sana Kwa Soka Letu.

Join the Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *