SINGIDA Black Stars imepanda kileleni mwa Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026 baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Mashujaa kwenye uwanja wa KMC.
Bao pekee la Singida BS limefungwa na mchezaji Elvis Rupia raia wa Kenya dakika ya 45+5 ya mchezo.

Ushindi huo unaifanya Singida BS kufikisha alama sita baada ya michezo miwili huku ikiwa haijaruhusu bao.
Mchezo wa pili ulipigwa saa 10:15 alasiri mkoani Mbeya uliozikutanisha Mbeya City dhidi ya Young Africans kwenye uwanja wa Sokoine na kumalizika kwa Suluhu.

Mchezaji Baraka Filemon wa Mbeya City alitajwa Kama Mchezaji Bora wa mchezo huo kutokana na mchango mkubwa aliotoa kwa timu yake kwenye mchezo huo.