IKIKAMILISHA mizunguko 14 Ligi ya Championship ya NBC imeendelea kuleta msisimko zaidi kutokana na ushindani wa timu zikipambana kupanda Ligi Kuu ya NBC huku nyingine zikipambana kusalia kwenye ligi hiyo kwa msimu unaofuata.
Utamu wa ligi hiyo upo zaidi kwenye nafasi ya kwanza na ya pili ambapo timu ya Geita Gold inashikilia usukani na Kagera Sugar ikishika nafasi ya pili huku timu hizo zikilingana alama (36), mabao ya kufunga (27), na mabao ya kufungwa (6).
Timu hizo zimeshacheza mchezo wao wa mzunguko wa kwanza ambapo zilitoka sare ya bao moja kwenye uwanja wa Nyankumbu, Geita ambapo timu ya Geita Gold ilikuwa mwenyeji.
Timu hizo za kutoka kanda ya ziwa hadi sasa ndio timu pekee kwenye ligi hiyo ambazo hazijapoteza mchezo wowote.
Timu za Hausung na Barberian zinashika nafasi mbili za chini zinazotoa timu za kushuka daraja zikikusanya alama saba kila mmoja huku timu hizo zikiwa zimepanda daraja na kushiriki ligi hiyo kwa mara ya kwanza msimu huu.
Timu ya B19 ndio timu iliyofungwa mabao mengi hadi sasa ikifungwa (27) ikiwa imeshinda michezo miwili pekee sawa na timu za Hausung na African Sports.
Timu ya Barberian inayoshika nafasi ya mwisho ndio timu iliyoshinda michezo michache msimu huu ikishinda mmoja pekee huku ikifanikiwa kufunga mabao nane pekee.
NDUGU MENEJIMENTI YA LIGI KUU TANZANIA
Napenda kuchukua nafasi hii Kuwasilisha maombi yangu ya kazi Katika oneo la utangazaji na maudhui ya soka.
Mimi ni miongoni mwa watu waliowahi kushiriki moja kwa moja katika utangazaji wa LIGI DARAJA LA KWANZA kipindi ambacho Ligi hiyo ilikua na mvuto mkubwa kwa mashabiki .
Tangu niondoke nimeendelea kufatilia maendeleo ya ligi zetu na kwa dhati ninaamini kuwa uzoefu wangu,ubunifu wa maudhui,na uelewa wa soka la Tanzania vinaweza kusaidia kuongeza mvuto, hadhira Na thamani ya ligi yetu ya championship
Nipo tayari kushilikiana Nanyi katika nafasi yeyote itakayo hitaji utaalamu wangu iwe ni utangazaji uhariri wa maudhui,au ubunifu wa vipindi vya soka ,
Naomba nipate fursa ya kuwasilaina Nanyi zaidi kwa maelezo ya kina au mahojiano .
ASANTENI KWA MUDA WENU.
Wenu mwaminifu.
Mussa mdaki