MAHESABU MAKALI ‘DAR DERBY’ LIGI KUU YA NBC LEO.

 

Ni vita ya mahesabu makali kwenye Mchezo wa ‘Derby’ ya Dar es salaam leo Machi 15, 2026 ambapo Azam FC itaialika Young Africans kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa saa 2:30 usiku.

Azam FC na Young Africans ndio timu pekee kwenye Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 ambazo hazijapoteza mchezo wowote hadi sasa katika michezo 13 timu hizo iliyocheza.

Kwenye eneo la ulinzi na ushambuliaji timu hizi zina namba nzuri zaidi kulinganisha na timu nyengine zinazoshriki Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

Kwa upande wa upachikaji mabao Young Africans imefunga jumla ya mabao 31 mengi zaidi kuliko timu yoyote ndani ya Ligi Kuu ya NBC ikifuatiwa na Azam FC iliyofunga mabao 21.

Kwenye eneo la Ulinzi Young Africans imeruhusu mabao mawili pekee machache zaidi kuliko timu yeyote inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC ikifuatiwa na Azam FC iliyofungwa mabao manne pekee.

Ushindi kwa Azam FC utaifanya kufikisha alama 30 na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC lakini pia kupunguza ‘pengo’ la alama na Kinara wa Ligi Kuu ya NBC Young Africans kwa alama tano (5).

Ushindi kwa Young Africans utaifanya iendelee kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa kufikisha alama 38 na kuendelea kuweka pengo kubwa la alama na wapinzani wake wa karibu.

Tukutane Benjamin Mkapa saa 2:30 usiku tushuhudie kipute cha Ligi Kuu ya NBC.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *