LIGI Kuu ya NBC itaendelea leo kwa michezo miwili itakayopigwa kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha ambapo timu ya TRA United itaikaribisha timu ya Simba na kwenyw uwanja wa Tanzanite Kwaraa mkoani Manyara Mbeya City itaialika timu ya Azam.
Michezo hiyo itakayochezwa saa kumi jioni ni muhimu kwa timu zote kutokana na timu hizo kutaka kujiweka nafasi nzuri ya kupambania ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.
TRA ipo nafasi ya nane katika msimamo ikicheza michezo 17 ushindi sita, sare tano na kufungwa michezo sita huku ikiwa imekusanya alama 23.

Kwa upande wa Simba iko nafasi ya pili kwenye msimamo ikicheza michezo 16 ushindi mechi 10 sare tano na kufungwa mchezo mmoja huku ikikusanya jumla ya alama 35.
Mchezo wa pili ni muhimu kwa Mbeya City ambapo timu hiyo inatafuta alama iweze kupanda zaidi katika eneo zuri huku Azam ikiwa katika mbio za ubingwa.

Mbeya City ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikicheza michezo 17 kushinda michezo minne, sare nne na kufungwa michezo tisa huku ikikusanya alama 16.
Kwa upande wa Azam ipo nafasi ya tatu ikicheza michezo 17 kwa kushinda michezo nane na sare tisa huku ikikusanya alama 33.
JILALA NZUMBI_nikiwa mambali hongela yanga kwa ushidi leo