LIGI Kuu ya NBC imeendelea kwa mchezo uliochezwa uwanja wa KMC majira ya saa Moja jioni Mkoani Dar es Salam uliozikutanisha KMC dhidi ya Tanzania Prisons na kumalizika
kwa Sare ya bao 1-1.
Kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi huku Tanzania Prisons wakitangulia kupata bao la mapema dakika ya tano kupitia kwa Jeremiah Juma.
Hata hivyo KMC walirejea mchezoni dakika ya 38 baada ya Adam Uledi kusawazisha kwa shuti lililowapa matumaini mashabiki wao.
Kipindi cha Pili kilikuwa na ushindani mkali kutoka pande zote mbili,kila timu ikitafuta bao la ushindi lakini safu za ulinzi zilisimama imara kuzuia mashambulizi ya timu pinzani.
Matokeo haya yanaacha hali ngumu kwa timu zote mbili katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC, KMC ikiongeza alama moja muhimu lakini bado haitoshi kuwatoa kwenye presha ya kushuka daraja wakiwa nafasi ya 16 na alama tisa huku wakihitaji ushindi katika michezo ijayo ili kujiweka salama.
Tanzania Prinsons nao wapo kwenye nafasi mbaya kwenye nafasi ya 15 baada ya kukusanya alama 14 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kwa matokeo hayo hakuna timu ambayo ipo salama na vita ya kuepuka kushuka daraja inaendelea kuwa kali kadri msimu unavyoelekea ukingoni huku michezo iliyosalia ikiwa na umuhimu mkubwa kwa timu hizo.