Ligi ya Championship imeendelea kwa michezo miwili iliyochezwa katika viwanja tofauti, huku mtibwa sugar na Bandari zikiibuka na ushindi wa kwanza msimu huu katika mechi za raundi ya pili .
Katika uwanja wa Manungu ulioko mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar imeifunga Mbuni mabao 2-1.
Mtibwa Sugar ilipata mabao yake kupitia kwa Musa Mpina aliyefunga yote mawili na Juma Luizio aliifungia Mbuni bao pekee.
Wakati huo katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma, Bandari imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gunners.
Bao la pekee la mchezo huo lilifungwa dakika ya 64 na John Simbe na kuiwezesha Bandari kuondoka na alama zote tatu ukiwa ushindi wa kwanza kwa timu hiyo kwenye Ligi ya Championship ya NBC.