TIMU za Simba na Tanzania Prisons zimetakata katika viwanja vya nyumbani baada ya kuibuka na ushindi katika michezo yao ya kukamilisha mzunguko wa 26.
Mchezo Simba na Pamba ulianza kwa kasi kila timu ikicheza kwa tahadhari kubwa ambapo ilimchukua dakika saba kiungo wa Simba, Ellie Mpanzu kufungua ukurasa wa mabao na dakika ya 18 Mathew Tegisi wa Pamba alisawazisha hivyo mchezo kwenda mapumziko wakiwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu kushambuliana na dakika ya 64 mchezaji wa Simba Libase Gueye aliipatia Simba bao la pili hivyo mpaka mchezo unatamatika Simba ilipata ushindi wa 2-1.
Kwa upande wa mchezo uliopigwa Sokoine timu ya Tanzania Prisons iliikaribisha Dodoma Jiji kwenye mchezo ulikuwa wa kushambuliana na dakika mbili zilimtosha Fransisco Lulihoshi kufungua akaunti ya magoli kupitia mkwaju wa penati .
Oscar Mwajanga aliiongezea bao la pili Prisons dakika ya 12 huku Waziri Junior wa Dodoma akifunga bao la kufutia machozi kwa timu yake dakika ya 43 hivyo kwenda mapumziko 2-1.
Kipindi cha pili kilirejeahuku Dodoma ikionekana kushambulia zaidina hata hivyo Oscar Mwajanga alizidi kudidimiza matumaini yao baada ya kufunga bao la 3 hivyo mchezo kuisha 3-1.