PAZIA LA FIRST LEAGUE LAFUNGWA.

Pazia la First League limefungwa jana kwa timu ya Rhino Rangers ya Tabora kufanikiwa kutwaa ubingwa wa First League msimu wa 2025/26 baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 4-2 dhidi ya Bandari kufuatia sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 90 za mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar.

 

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku Rhino Rangers wakitangulia kupata bao kupitia Iddy Manyerere dakika ya 6.

 

Bandari walijibu dakika ya 10 kupitia Mussa Ally kabla Iddy Manyerere kuongeza tena la pili dakika ya 40 na kuirejeshea Rhino Rangers uongozi wa 2-1 kabla ya mapumziko.

 

Bandari walionyesha mapambano makubwa kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 89 kupitia Benedicto Jacob na kuufanya mchezo kumalizika kwa sare ya 2-2 ndani ya muda wa kawaida.

 

Katika mikwaju ya penalti, Rhino Rangers walikuwa watulivu na makini zaidi wakishinda kwa mabao 4-2 na kutwaa taji la First League 2025/26 mbele ya mashabiki.

 

Ushindi huo unahitimisha msimu mzuri kwa Rhino Rangers ambao wameonyesha uimara, nidhamu na uthabiti katika safari yao ya kutwaa ubingwa wa First League.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *