PAMBA, YANGA, PRISONS ZATEMBEZA ‘DOZI’ LIGI KUU YA NBC.

 

Michezo mitatu ya raundi ya 27 ya Ligi Kuu ya NBC imechezwa jana katika viwanja tofauti huku mechi zote zikichezwa muda mmoja wa saa 10:00 alasiri huku Pamba Jiji , Yanga na Tanzania Prisons zikiibuka na ushindi muhimu.

Katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Pamba Jiji imepata ushindi mnono kwa kuichapa Mtibwa Sugar mabao 4-0 huku mshambuliaji Methew Tegis akiwa nyota wa mchezo baada ya kufunga (hat-trick) katika dakika za 17, 46 na 48, na Shaphan Siwa akifunga bao lingine dakika ya 43.

Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ulishuhudia Yanga ikiendeleza mwenendo wake mzuri kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate.

Pacome Zouzou aliifungia Yanga bao la kwanza mapema kipindi cha pili kabla ya Laurindo Depu kuongeza la pili na kuhakikisha ‘Wananchi’ wanaondoka na Alama zote tatu.

Nako kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Tanzania Prisons iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye uwanja wa ugenini.

Bao pekee la mchezo lilifungwa na George Mpole dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati.

Matokeo hayo yanaendelea kuongeza ushindani katika Ligi Kuu ya NBC huku kila timu ikisaka kutimiza malengo yake kabla ya msimu wa 2025/26 kufikia tamati.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *