LIGI ya Championship ya NBC championship 2026/27 imeanza kwa ushindi wa kuvutia baada ya timu tatu za KMC,Kigamboni na Rhino Rangers kuanza kwa kupata ushindi.
KMC ilianza kwa kishindo baada ya kuichapa Mbuni mabao 5-1 katika mchezo uliochezwa LKMC complex huku ushindi huo ukiwa kwa hisani ya mabao ya Ramadhan Kalanje, Frank ikobela, Salum Mlemwa, Abdallha Madirisha na Adam Uledi.
Katika uwanja wa uhuru,Kigamboni united ilianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya ‘maafande’ wa TMA kutoka Arusha.
Nicodemus Ntarema ndiye aliyekuwa shujaa wa Kigamboni baada ya kufunga bao pekee la mchezo dakika ya 33 na kuipa timu yake alama tatu muhimu za mwanzo wa msimu.
Rhino Rangers ilianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliochezwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.
Zuberi Malila aliipa Rhino Rangers bao la ushidi dakika ya 13 na timu hiyo ikafanikiwa kulinda bao hilo mpaka mwisho na kuondoka na alama tatu muhimu.