KMC YANG’ARA; TRANSIT CAMP NA KENGOLD ZAVUNA ALAMA TATU.

Ligi ya championship ya NBC msimu wa 2026/27 uliendelea jana, kwa michezo ya raundi ya pili ambapo jumla ya mechi nne zilichezwa katika viwanja mbalimbali zote zikianza saa 10:00 jioni.

Katika uwanja wa Uhuru,Dar es saalam Transit Camp ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TMA Stars. Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Kalegea Murusu Mazanga dakika ya 59 na kuihakikishia Transit Camp alama tatu muhimu.

Mkoani Tanga,katika uwanja wa Mkwakwani,KMC iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bigman.

KMC ilianza kupata bao la kupitia Ramadhani Kalanje dakika ya 45, kabla ya mchezaji huyo kuongeza la pili kwa mkwaju wa Penati dakika ya 66.

Bigman ilirejea kwa nguvu na kupata bao la kwanza kupitia kwa Kelvin John Kayongo aliyefunga kwa penati dakika ya 71,kabla Adam Uledi wa KMC kukamilisha ushindi huo kwa kufunga bao la tatu dakika ya 77.

Mkoani Ruvuma, katika uwanja wa Majimaji Songea United na Rhino Rangers zilitoka sare 0-0 hivyo kila timu ikaondoka na alama moja.

Katika mchezo mwingine Kengold ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya IAA katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa manispaa ya Chunya, Kengold ilifunga mabao mawili na kuondoka na alama zote tatu huku IAA ikishindwa kupata chochote katika mchezo huo.

Hadi sasa timu zote zimecheza michezo miwili, KMC ikiongoza ligi hiyo kwa alama sita sawa na timu ya Stand United na ‘wana kino Boys’ wakikaa juu kwa tofauti ya mabao.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *