
KIUNGO Mshambuliaji wa timu ya Simba inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC Clatous Chama amezidi kuonyesha umahiri wa mguu wake wa kulia baada ya kufunga mabao manne kwa mguu huo.
Mabao hayo aliyapata katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji uliochezwa CCM Kirumba, Mwanza, Singida Black Stars katika uwanja wa Airtel mkoani Singida, dhidi ya Geita Gold katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na mchezo wa dabi ya Mzizima dhidi ya Azam katika uwanja wa Azam Complex huku akiwa ametumia dakika 440 .
Maxi Nzengeli wa Young Africans amefanikiwa kufunga mabao matatu kwa mguu wake wa Kulia katika mechi dhidi ya Namungo katika uwanja wa Majaliwa, dhidi ya Pamba Jiji kwenye uwanja wa KMC Complex na dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa KMC ikiwa ametumia dakika 521.

Maabad Maabad wa Coastal Union amefunga mabao matatu kwa mguu wa kulia ikiwa ametumia dakika 475 katika mechi dhidi ya Polisi Tanzania alipofunga mabao mawili katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na dhidi ya JKT Tanzania katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Abdul Suleiman wa Azam alifanikiwa kufunga mabao hayo katika mechi dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, dhidi ya TRA United mchezo uliochezwa Azam Complex Dar es Salaam na Geita Gold katika uwanja wa Bukombe akiwa ametumia dakika 297.