OSEJA KINARA WA ‘KUFUTA’ PENATI ZA LIGI KUU YA NBC.

GOLIKIPA wa timu ya Kagera Sugar, Adam Oseja, ameonyesha ubabe wake baada ya kufanikiwa kupangua penati mbili ndani ya mizunguko sita ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027.

Oseja ameokoa penati ya mchezaji wa Mashujaa, Salum Kihimbwa, katika mchezo wa Mashujaa dhidi ya Kagera akifanikiwa pia kupangua mkwaju wa Iddy Selemani wa Azam katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Kagera Sugar na Azam huku kipa huyo akiwa amedaka michezo miwili sawa na dakika 180.

Chuma Ramadhani wa Coastal Union amecheza michezo mitano hadi sasa sawa na dakika 438 na golikipa huyo alifanikiwa kuokoa penati iliyopigwa na mchezaji wa Mashujaa, Mishamo Daudi, katika mchezo wa Coastal Union dhidi ya Mashujaa uliochezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Frank Faustine wa Geita Gold amefanikiwa kuokoa penati iliyopigwa na mchezaji wa Namungo Awesu Awesu katika mchezo wa Namungo dhidi ya Geita Gold uliochezwa katika uwanja wa Majaliwa Lindi huku kipa huyo akiwa amekaa langoni michezo sita sawa na dakika 540.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *