KHALEBI KINARA WA MABAO CHAMPIONSHIP.

Mshambuliaji Abiudy Khalebi wa Mbeya kwanza ameanza kuonyesha ‘makucha’ yake kwenye suala la kucheka na ‘nyavu’ akiwa ndiye kinara wa wafungaji katika Ligi ya Championship ya NBC hadi sasa akifunga mabao manne.

Khalebi anaongoza orodha hiyo akifuatiwa na wachezaji wawili wa KMC Adam Uledi na Ramadhani Kalanje ambao kila mmoja amefunga mabao matatu.

Nyuma yao kuna kundi la wachezaji waliokwisha kufunga mabao mawili akiwemo Oscar Paul wa Tanzania Prisons, Juma Liuzio wa Mtibwa Sugar, Hamdani Ally wa Transit Camp na Zuberi Malila wa Rhino Rangers.

KMC ndiyo timu yenye wachezaji wawili katika nafasi za juu huku Uledi na karanje wakiwa wamefunga mabao matatu kila mmoja, pia imeanza msimu kwa kasi ikishinda michezo yake yote ya mwanzo mitatu na kufunga mabao 11 katika michezo mitatu.

Kalanje tayari ameonyesha uwezo wake wa kufunga tangu mwanzo wa msimu akianza kampeni hiyo katika mchezo wa kwanza wa ligi hiyo dhidi ya Mbuni.

Kwa upande wa Zuberi Malila, alifunga bao katika ushindi wa bao moja dhidi ya Mtibwa Sugar mwanzo wa msimu.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *