Ligi ya Championship itaendelea leo mzunguko wa nne katika mikoa mitatu huku michezo yote ikianza saa 10:00 alasiri na kuchezwa mkoani Mbeya, Dar es saalam na Arusha.
TMA itakuwa mwenyeji wa Bigman kwenye uwanja wa wa Sokoine huku TMA ikiingia kwenye mchezo huo na hitaji la kupata matokeo baada ya mechi yake dhidi ya Stand United kuahirishwa katika mzunguko uliopita.
Dar es saalam Transit Camp itakuwa mwenyeji wa IAA kwenye uwanja wa uhuru. Transit Camp imeanza msimu ikiwa miongoni mwa timu zinazofanya vizuri huku IAA ikionyesha ushindani katika michezo yake ya mwanzo na mchezo huu utaonyeshwa moja kwa moja kupitia Ligi Kuu TV kwenye mtandao wa Youtube.
Mchezo mwingine utachezwa mkoani Arusha ambapo Mbuni itakuwa mwenyeji wa Gunners kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid huku kila timu ikihitaji kusaka alama na mchezo huu utaonyeshwa kupitia chaneli ya FIFA+.