KMC YAISAKA NAFASI LIGI KUU 2026/2027.

Mzunguko wa nne wa mechi za Ligi ya Championship ya NBC umetamatika katika viwanja mbalimbali nchini huku kila timu ikipambana kuhakikisha inacheza vyema mechi zake kujiweka nafasi nzuri.

KMC inashika usukani kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC huku ikiwa imecheza mechi nne na kuchukua alama 10, timu hiyo imefunga mabao 12 na kuruhusu mabao matatu.

Transit Camp ipo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC ikiwa imecheza mechi nne, imetoa sare mchezo mmoja na kushinda michezo mitatu huku ikikusanya alama 10, timu hiyo imefungwa mabao matatu na kufunga mabao saba.

Nafasi ya tatu ipo timu ya Tanzania Prisons timu hiyo imecheza mechi nne, ushindi tatu, kupoteza mchezo mmoja na timu hiyo ndani ya msimu huu imefunga mabao matano, kufungwa mabao mawili na kuweza kukusanya alama tisa.

Stand United ipo nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC ikiwa imecheza michezo mitatu, imeshinda michezo yote mitatu, imefunga mabao manne na imeruhusu bao moja huku ikukusanya alama tisa.

Kigamboni United ipo katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC huku ikiwa imecheza michezo minne, imeshinda mechi mbili, sare moja, na kupoteza mchezo mmoja.

Timu hiyo imefunga mabao manne,imeruhusu mabao matatu na imeweza kukusanya alama saba.

Mtibwa Sugar inashika nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC, imecheza michezo minne huku ikishinda mechi mbili sare moja na kupoteza mchezo mmoja timu hiyo ina mabao manne imeruhusu mabao matatu imekusanya alama saba.

Rhino Rangers inashika nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC, timu hiyo imecheza michezo minne, sare moja na kushinda michezo miwili kufungwa mmoja huku timu hiyo imeweza kufunga mabao mawili na kuruhusu bao moja, ikiweza kukusanya alama saba.

Bandari Tanzania ipo katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC timu hiyo imecheza michezo minne, kushinda mchezo mmoja, sare mechi mbili na kupoteza mchezo mmoja aidha imefanikiwa kufunga mabao manne kufungwa mabao manne huku ikiwa imekusanya alama tano.

KenGold inashika nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC imecheza michezo minne, imeshinda mchezo mmoja sare moja na kupoteza michezo miwili aidha timu hiyo imefunga mabao manne, imeruhusu mabao sita na imevuna alama nne.

IAA iashika nafasi ya kumi katika msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC timu hiyo imecheza mechi nne imeshinda mchezo mmoja, sare moja na kupoteza michezo miwili, aidha imefanikiwa kufunga mabao matatu kufungwa mabao sita na kukusanya alama nne.

Songea United ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC imecheza mechi nne, sare michezo mitatu kufungwa mmoja aidha timu hiyo imefunga bao moja, kufungwa mabao mawili na imevuna alama tatu.

Mbeya Kwanza inashika nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC, timu hiyo imecheza michezo minne imeshinda mchezo mmoja imepoteza michezo mitatu na imefunga mabao manne, imefungwa mabao sita huku ikikusanya alama tatu.

Mbuni ndio inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC, timu hiyo imecheza michezo minne ushindi mmoja, kupoteza michezo mitatu ikiwa imefunga mabao manne imefungwa mabao tisa na ikivuna alama tatu.

Gunners ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC timu hiyo imecheza michezo minne, sare mbili, imepoteza michezo miwili, imefunga mabao mawili na kufungwa mabao matano imefanikiwa kukusanya alama mbili.

TMA inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC, timu hiyo imecheza michezo mitatu na kupoteza michezo yote miwili na sare moja aidha imefungwa mabao manne kufunga mabao mawili na kuvuna alama moja.

Bigman ipo nafasi ya 16 na ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC imecheza michezo minne na imepoteza michezo mitatu sare moja ikiwa imefunga mabao matano na kufungwa mabao saba huku ikivuna alama moja.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *