TIMU ya Simba ‘imeshindikana’ ndani ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027 baada ya kucheza michezo saba pasipo kupoteza mchezo wowote.
Simba imeshinda michezo yote hiyo na kuweza kukusanya alama 21, kufunga mabao 13 na kuruhusu mabao matatu ndani ya msimu huu.
Young Africans ndio inafuatia baada ya kucheza michezo saba huku timu hiyo ikishinda mechi sita na kufungwa mchezo mmoja aidha timu hiyo imefunga mabao 17 ikiruhusu mabao manne tu na kuweza kukusanya alama 18.
Azam imecheza michezo nane ikishinda michezo mitano kufungwa mmoja na sare mbili huku timu hiyo ikiweza kukusanya alama 17 kufunga mabao 13 na kufungwa mabao saba.
Mashujaa imeweza kucheza michezo saba ushindi nne na kufungwa tatu aidha timu hiyo imefunga mabao nane kufungwa moja na kukusanya alama 12.
Singida Black Stars amecheza michezo nane, ushindi tatu, sare mbili na kupoteza michezo mitatu huku timu hiyo ikifunga mabao 14 kufungwa 11 na kukusanya alama 11.
Dodoma Jiji imecheza michezo saba ushindi tatu, sare mbili na kufungwa michezo miwili, aidha timu hiyo imeweza kufunga mabao Matano kufungwa Matano na kukusanya alama 11.
Polisi Tanzania, Mbeya City, JKT Tanzania zimecheza michezo saba ushindi michezo mitatu, sare moja na kufungwa michezo mitatu kila timu huku ikikusanya alama 10.
Coastal Union na Namungo wamecheza michezo nane kila timu ushindi michezo mitatu, sare moja kwa Coastal Union huku Namungo akiwa bado hana sare, Coastal imepoteza michezo minne Coastal na Namungo mitano, Coastal ikikusanya alama 10 na Namungo alama tisa.
Geita Gold imecheza michezo saba ushindi michezo miwili sare moja na kufungwa michezo minne huku ikikusanya alama saba.
TRA United na Kagera Sugar zimecheza michezo saba kila timu huku zikishinda mchezo mmoja, sare tatu kwa TRA, mbili kwa Kagera, kufungwa tatu kwa TRA na kufungwa michezo minne Kagera Sugar aidha TRA imekusanya alama sita na Kagera ikikusanya alama tano.
Pamba Jiji na Fountain Gate zimecheza michezo saba ushindi mchezo mmoja kila timu sare moja na kufungwa michezo mitano aidha timu hizo zimekusanya alama nne kila mmoja.