ANUARY KINARA WA MABAO LIGI KUU NBC.

Mshambuliaji wa timu ya Polisi Tanzania Anuary Jabir hacheki na yeyote kwenye suala la kutupia mabao nyavuni ndani ya Ligi Kuu ya NBC akiwa ndiye kinara wa mabao hadi sasa baada ya kufunga sita.

Jabir ambae amecheza michezo saba mpaka sasa sawa na dakika 562 amefanikiwa kufunga mabao hayo na akitoa pasi saidizi moja ndani ya Ligi Kuu ya NBC.

Peter Shalulile wa timu ya Young Africans ndie mchezaji anaefuatia ‘akichana’ nyavu za wapinzani mara nne, pasi saidizi moja katika michezo sita aliyocheza sawa na dakika 478.

Clatous Chama wa Simba ambaye amecheza dakika 502 sawa na michezo sita amefanikiwa kufunga mabao manne ndani ya Ligi Kuu ya NBC.

Obrey Chirwa wa Geita Gold amefanikiwa kucheza michezo mitano sawa na dakika 360 na kufanikiwa kufunga mabao manne hadi sasa.

Abdul Suleiman ‘Sopu’ wa Azam nae hayuko mbali amefanikiwa kufunga mabao manne akicheza michezo mitano sawa na dakika 297.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *