‘HASHIKIKI’ hivyo ndivyo unaweza kumueleza kiungo wa timu ya Simba Libasse Gueye ambaye ni kinara wa pasi saidizi za mabao ndani ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027.
Mchezaji huyo ambaye ni msimu wake wa pili ndani ya timu ya Simba amefanikiwa kutoa pasi saidizi saba na kufunga mabao mawili ndani ya michezo nane ambayo ni sawa na dakika 626 alizocheza Ligi Kuu ya NBC.
Housseine Zakouani ni kiungo wa timu ya Young Africans ikiwa ni msimu wake wa kwanza ndani ya timu hiyo amecheza dakika 255 kakika michezo mitano ya Ligi Kuu ya NBC amefanikiwa kutoa pasi saidizi tatu hadi sasa.
Jeancy Kinda wa Singida Black Stars ni msimu wake wa kwanza akiwa na timu hiyo amecheza michezo nane sawa na dakika 625 na kufanikiwa kutoa pasi saidizi tatu huku akifunga bao moja.
Valentino Mashaka (JKT Tanzania), Hassan Mubiru (Azam), Max Nzengeli, Albert Kangwanda na Chadrack Boka (Young Africans), Anicet Oura (Simba), Henry David na Yusuph Khamis (Singida), Haruni Chanongo na Crispin Ngushi (Mashujaa), Vicent Abubakar (Geita Gold), Yassin Salehe (Kagera Sugar) na Osca Mwajanga wa Mbeya City wachezaji hao wamefanikiwa kutoa pasi saidizi mbili ndani ya Ligi Kuu ya NBC.