SIMBA KINARA WA MABAO LIGI KUU YA NBC.

 

Simba inaongoza kwa idadi ya mabao yaliyofungwa katika ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27 ikiwa ‘imefumania’ nyavu mara 19 na kuruhusu mabao manne katika michezo nane iliyocheza.

Watani zao wa jadi Yanga wanaendelea kuwafukuzia kwa karibu wakiwa wamefunga mabao 17 na kuruhusu manne katika michezo saba. Hali hiyo inaifanya mbio za timu hizo mbili katika safu ya ushambuliaji kuwa miongoni mwa mambo yanayovutia huku Yanga ikiwa na mchezo mmoja pungufu ya Simba.

Singida black Stars inashika nafasi inayofuata kwa kufunga mabao 14 na kuruhusu 11 katika michezo nane huku Azam ikiwa imefunga mabao 13 na kuruhusu saba katika michezo nane.

Katika timu zilizofunga mabao tisa ni Mashujaa katika michezo nane huku ikiruhusu 13 wakati Jkt Tanzania na Geita Gold zimefunga idadi hiyo katika michezo saba kila mmoja na zikifungwa mabao 11.

Polisi Tanzania imefunga mabao 10 na kuruhusu tisa katika michezo saba, Pamba Jiji ikiwa na mabao manane ya kufunga, 13 ya kufungwa katika michezo saba.

Mbeya City, Coastal Union na Namungo zimefunga mabao saba kila mmoja, Mbeya City imeruhusu mabao saba katika michezo saba,huku Coastal Union na Namungo zikiruhusu 11 kila mmoja katika michezo nane.

Kwa upande mwingine TRA United imefunga mabao sita na kuruhusu saba katika michezo saba, huku Dodoma Jiji ikiwa na mabao matano ya kufunga na matano ya kufungwa katika michezo saba.

Kagera Sugar imefunga mabao manane na kuruhusu 15 katika michezo saba, wakati Fountain Gate ikiwa na mabao matatu na kufungwa 11 katika michezo saba.

Kadiri Ligi inavyoendelea kila timu itakuwa na nafasi ya kuboresha na kubadilisha mwelekeo wa ushindani.

Je Simba itaendelea kuongoza kwa mabao au Yanga na wapinzani wengine wataongeza kasi katika raundi zijazo?

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *