JKT YAICHAPA MBEYA CITY LIGI KUU YA NBC.

Ligi Kuu ya NBC imeendelea mzunguko wa nane ikiwakutanisha JKT Tanzania dhidi ya Mbeya City na
JKT kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo saa 1:00 jioni.

Mchezo huo ulianza kwa ushindani huku timu zote zikisaka nafasi ya kupata mabao ya mapema kabla ya JKT kuvunja ukimya dakika ya 45 +3 kupitia Valentino Mashaka aliyefunga bao la kwanza na kuifanya timu kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilirejea kwa timu zote kuendelea kupambana huku JKT ikifanikiwa kuongeza bao la pili dakika ya 88 kupitia Magata Fredrick na kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata ushindi.

Hata hivyo Mbeya City iliendelea kupambana hadi dakika za mwisho na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 90+3 kupitia Joseph Mabaga.

Matokeo hayo yanaifanya JKT kuondoka na alama zote tatu katika mchezo huo na mchezaji bora wa mchezo huo alikuwa Valentino Mashaka wa JKT Tanzania.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *