ANUARY HASHIKIKI UFUNGAJI BORA LIGI KUU YA NBC.

MSHAMBULIAJI Anuary Jabiri wa Polisi Tanzania ameendelea kung’ara katika mbio za kuwania kiatu cha ufungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027, akiwa kinara wa orodha hiyo kwa sasa kwa kufikisha mabao saba.

Jabiri amekuwa na mwanzo mzuri wa msimu, akijitengenezea nafasi ya kuongoza orodha ya wafungaji akiwa amecheza michezo tisa sawa na dakika 889 amefanikiwa kuingia nyavuni mara saba.

Mshambuliaji wa Young Africans, Peter Shalulile, anafuata katika orodha hiyo baada ya kuingia wavuni mara sita katika dakika 670 alizocheza ndani ya michezo tisa.

Harbet Lukindo wa Namungo ndio anaefuata akiwa ametumia dakika 479 ndani ya michezo nane kuhakikisha anafunga mabao matano ndani ya msimu wa 2026/2027 wa Ligi Kuu ya NBC.

‘Mkongwe’ Obrey Chirwa wa Geita Gold amecheza dakika 702 kwenye michezo tisa ya Ligi Kuu ya NBC amefanikiwa kufunga mabao matano hadi sasa.

Clatous Chama, wa timu ya Simba mpaka sasa amefanikiwa ‘kuchana’ nyavu za wapinzani mara nne akitumia dakika 661 ndani ya michezo tisa ya ligi hiyo.

Elie Mpanzu wa timu ya Simba ametumia dakika 708 ndani ya michezo 10 akifanikiwa kufunga mara nne.

Anicet Oura wa Simba hayuko mbali na wenzake amefanikiwa kufunga mabao manne akitumia dakika 809 ndani ya michezo 10 ya ligi Kuu ya NBC.

Wachezaji wengine wenye idadi hiyo ni Ani Elijah wa TRA United nae amefanikiwa kufunga mabao manne akitumia dakika 567 katika michezo 9 aliyocheza.

Abdul Suleiman timu ya Azam amecheza michezo saba msimu huu akitumia dakika 384 kupata mabao manne ndani ya Ligi Kuu ya NBC.

Ushindani huo unaashiria vita kali ya kuwania kiatu cha ufungaji bora msimu huu, huku kila mshambuliaji akitazamiwa kutumia michezo inayofuata kuongeza idadi ya mabao na kujiimarisha katika orodha hiyo.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *