Michezo miwili ya NBC Championship msimu wa 2026/27 iliendelea mzunguko wa tisa na kushuhudia Bigman ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Songea United, huku KMC na Rhino Rangers zikigawana alama kwa sare ya 1-1.
Katika mchezo uliochezwa uwanja wa CCM mkwakwani majira ya saa 10:00 jioni, Bigman ilianza kwa kupata bao la kwanza dakika ya 27 kupitia kwa Baraka Said kabla ya Ayubu Abdallah kuongeza bao la pili dakika ya 78 na kuhitimisha ushindi huo muhimu nyumbani.
Katika mchezo mwingine,KMC na Rhino Rangers zilitoka sare katika mpambano uliokuwa na ushindani mkali, mchezo uliochezwa uwanja wa KMC jijini Dar es saalam majira ya saa 10:00jioni
Ramadhani Hashimu Kalanje iliipa KMC bao la kuongoza ,lakini Rhino Rangers ilirejea mchezoni kupitia elias Maguli aliyefunga bao la kusawazisha dakika ya 66 na kufanya timu hizo kugawana alama moja moja.
KMC inaongoza kwenye msimamo wa ligi ya NBC Championship ikiwa na alama 19 na ikishika nafasi ya kwanza huku Rhino Rangers ikiwa nafasi ya nne na alama 15.
Matokeo hayo yanaifanya Bigman kuvuna alama tatu muhimu kwenye mchezo wa pili mfululizo huku KMC na Rhino Rangers kila moja ikiongeza alama moja.