KMC YANG’ANG’ANIA KILELENI LIGI YA CHAMPIONSHIP YA NBC.

LIGI ya Championship ya NBC 2026/2027 imeendelea kushika kasi ikiwa ni mzunguko wa tisa wa ligi hiyo huku timu zote 16 zikiwa zimeshiriki kikamilifu katika viwanja tofauti ili kujitafutia alama kwenye mizunguko yote.

KMC ya Dar es Salaam inaongoza msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC ikiwa imecheza michezo tisa bila kupoteza mchezo wowote. KMC imeshinda michezo mitano,sare nne, imefunga mabao 17 na kuruhusu mabao sita huku ikivuna alama 19.

Mtibwa Sugar ya Morogoro inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC, ikiwa imecheza michezo tisa na kushinda michezo mitano, sare tatu na kupoteza mchezo mmoja, imefunga mabao 10 na kuruhusu mabao sita ikikusanya alama 18.

Tanzania Prisons ya mkoani Mbeya inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi ya NBC Championship, ikiwa imecheza michezo tis na kushinda michezo mitano, sare michezo miwili na kupoteza michezo miwili ikiwa imefunga mabao 14 na kuruhusu mabao sita ina alama 17 kwenye msimamo.

Bandari Tanzania ya Mtwara iliyopanda daraja inashika nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa imecheza michezo tisa na kushinda michezo mitano, sare mbili na kupoteza michezo miwili imefunga mabao 12 na kuruhusu mabao matano ina alama 17.

Rhino Rangers ya mkoani Tabora inashika nafasi ya tano katika msimamo ikiwa imecheza michezo tisa, na kupata ushindi kwenye michezo minne, sare tatu na kupoteza michezo miwili aidha timu hiyo imefunga mabao saba na kuruhusu mabao nane ina alama 15.

Stand United ya Shinyanga inashika nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC ikiwa imecheza michezo tisa, na kupata ushindi wa michezo minne, sare michezo miwili na kupoteza michezo mitatu pia imefunga mabao 11 na kuruhusu 10 ina alama 14.

Transit Camp kutoka Dar es Salaam ipo nafasi ya saba kwenye msimamo baada ya michezo tisa iliyocheza, imeshinda michezo minne, sare mchezo mmoja na kupoteza michezo minne pia imefunga mabao 15 na kuruhusu mabao 13 ina alama 13.

Kigamboni United ya Dar es Salaam inashika nafasi ya nane katika msimamo baaada ya kuwa imecheza michezo tisa na kushinda michezo mitatu, sare michezo mitatu na kupoteza michezo mitatu aidha imefunga mabao tisa na kuruhusu mabao nane ina alama 12.

Gunners ya Dodoma inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo baada ya kucheza michezo tisa na kupata ushindi katika michezo miwili, sare michezo mitano na kupoteza michezo miwili aidha imefunga mabao saba na kuruhusu mabao saba ikiwa na alama 11.

IAA ya Arusha inashika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi hiyo baada ya kuwa imecheza michezo tisa na kupata ushindi katika michezo miwili, sare michezo mitano na kupoteza michezo miwili aidha imefunga mabao tisa na kuruhusu mabao 11 ikiwa na alama 11.

Mbuni ya Arusha inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC baada ya kushuka dimbani mara tisa na kupata ushindi katika michezo mitatu, sare michezo miwili na kupoteza michezo minne aidha imefunga mabao 12 na kuruhusu mabao 16 na imekusanya alama 11.

Bigman ya Tanga inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC baada ya kushuka dimbani mara tisa na kupata ushindi wa michezo mitatu, sare mchezo mmoja na kupoteza michezo mitano aidha imefunga mabao 12 na kuruhusu mabao 16 imekusanya alama 10.

KenGold ya Mbeya inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo tisa na kupata ushindi katika michezo miwili, sare michezo mitatu na kupoteza michezo minne aidha imefunga mabao 11 na kuruhusu mabao 14 imekusanya alama tisa.

Tabora United ya mkoani Tabora inashika nafsi ya 14 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo tisa na kupata ushindi katika michezo miwili, sare moja na kupoteza sita aidha imefunga mabao 10 na kuruhusu mabao 15 imekusanya alama saba.

Songea United ya mkoani Ruvuma inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo tisa na kupata ushindi kwenye mchezo mmoja, sare michezo mitatu na kupoteza michezo mitano aidha imefunga mabao manne na kuruhusu mabao 11 imekusanya alama sita.

TMA ya Iringa inashika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC baada ya kuwa imecheza michezo tisa na kupata ushindi wa mchezo mmoja, sare michezo miwili na kupoteza michezo sita aidha imefunga mabao matatu na kuruhu mabao 15, imekusanya jumla ya alama mbili.

Timu hiyo ilikatwa alama tatu pamoja na kupoteza mchezo baada ya kushindwa kufika uwanjani kwenye mchezo wake dhidi ya Stand United

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *