ANUARY MKALI WA MIKWAJU YA PENATI LIGI KUU YA NBC

MSHAMBULIAJI wa timu ya Polisi Tanzania Anuary Jabiri hashikiki kwenye kufunga mabao ya mkwaju wa penati ndani ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027.

Mkali huyo amefunga mabao manne ya mkwaju wa penati katika mechi za Polisi Tanzania dhidi ya Azam katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha, Polisi Tanzania dhidi ya Pamba Jiji, Mashujaa dhidi ya Polisi katika uwanja wa Lake Tanganyika na Polisi dhidi ya Mbeya City.

Abdul Suleiman wa Azam ndio anafuatia akifanikiwa kuweka mabao matatu ya mkwaju wa penati nyavuni katika michezo ya Polisi dhidi ya Azam katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha, Azam dhidi ya Pamba Jiji mchezo uliofanyika Azam Complex Dar es Salaam na Geita Gold dhidi ya Azam katika uwanja wa Bukombe mkoani Geita.

Obrey Chirwa wa Geita Gold amefunga mabao ya penati matatu katika michezo ya Geita Gold dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Bukombe, Geita dhidi ya Azam uwanja huo huo na mchezo wa TRA dhidi ya Geita Gold uliochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Maabad Maabad wa Coastal Union ameweka mikwaju ya penati katika michezo kati ya Coastal na JKT Tanzania uliochezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga na Coastal Union dhidi Polisi Tanzania uliochezwa Mkwakwani Tanga.

Rushine De Reuck wa Simba amefanikiwa kufunga mikwaju ya penati katika michezo ya Singida dhidi ya Simba uwanja wa Airtel mkoani Singida na Simba dhidi ya Namungo katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *