LIGI Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027 ilianza tarehe 14 Agosti ambapo timu tofauti zilikutana katika viwanja tofauti na kuonyesha umahiri wao, huku Simba ikiwa timu pekee iliyoshinda michezo kumi mfululizo hadi sasa.
Mechi yao ya kwanza kwenye msimu huu ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa Agosti 16 kwenye uwanja wa Kaitaba uliopo Kagera ambapo Simba ilishinda 0-2 mabao ya Simba yalifungwa na Elie Mpanzu na Ismael Toure.
Mchezo wa pili Simba ilicheza na Pamba jiji katika uwanja wa CCM Kirumba uliopo Mwanza ambapo Simba ilikuwa ugenini na ilishinda 1-2, mabao ya Simba yalifungwa na Anicet Oura na Clatous Chama huku bao la Pamba likifungwa na Idris Diomande.
Mchezo wa tatu Simba ilikuwa ugenini mkoani Singida katika uwanja wa Airtel ambapo ilifanikiwa kushinda 1-2 mabao ya Simba yalifungwa na Rushine De Reuck kwa mkwaju wa penati na Clatous Chama huku bao la Singida likifungwa na Shekhan Ibrahim.
Simba ilicheza na Coastal Union ikiwa ni mchezo wa nne katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Dar es Salaam ambapo ilishinda 1-0 bao hilo lilifingwa na Ismael Toure.
Katika mchezo wa tano Simba ilicheza na Geita Gold katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Dar es Salaam ambapo timu hiyo ilishinda 2-0 mabao hayo yalifungwa na Clatous Chama na Libasse Gueye.
Simba alikuwa mgeni wa Azam katika mchezo wa Dabi ya Mzizima kwenye uwanja wa Azam Complex Dar es Saalam ambapo ilishinda 0-2 mabao ya Simba yalifungwa na Clatous Chama na Azam walijifunga.
Simba ilikuwa mwenyeji wa Young Africans katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Saalam ambapo ilishinda 2-1 mabao ya Simba yalifungwa na Neo Maema na Elie Mpanzu huku bao la Young Africans lilifungwa na Peter Shalulile.
Simba ilicheza na Mashujaa katika mchezo wake wa nane kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na kushinda 6-1 mabao ya Simba yalifungwa na Elie Mpanzu mawili , Libasse Gueye , Morice Abraham, Anicet Oura na Ismael Toure huku bao la Mashujaa likifungwa na Selemani Bwenzi.
Simba ilikuwa ugenini mkoani Manyara katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa kuikabili timu ya Foutain Gate ambapo ilishinda 0-1 bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na beki wa Simba Rushine De Reuck.
Simba ilikuwa mwenyeji wa Namungo katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam ambapo ilishinda 3-2 mabao ya Simba yalifungwa na Anicet Oura mabao mawili, Rushine De Reuck moja huku mabao ya Namungo yakifungwa na Raymond Lulendi.