Kiungo wa timu ya Simba, Libasse Gueye, anaendelea kuonyesha ubora wake katika msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kuhusika katika mabao mengi kuliko mchezaji yoyote ndani ya Ligi hiyo.
Gueye anaongoza akiwa amehusika katika mabao tisa, ambapo amefunga mabao mawili na kutoa pasi saidizi saba ndani ya mizunguko 10 ya Ligi Kuu ya NBC.
Anuary Jabiri wa timu ya Polisi Tanzania mwenye ushiriki wa mabao nane ambapo amefunga mabao saba na kutoa pasi saidizi moja .
Nafasi ya tatu inashikiliwa na Ani Elijah wa timu ya TRA akifanikiwa kuweka nyavuni mabao manne na kutoa pasi saidizi tatu katika michezo ya Ligi Kuu ya NBC.
Peter Shalulile wa timu ya Young Africans nae hacheki na wapinzani kwani amefanikiwa kufunga mabao sita ka kutoa pasi saidizi moja sawa na kuhusika katika mabao saba.
Mchezaji mwingine aliyehusika katika mabao mengi ni winga wa timu ya Simba Ellie Mpanzu akifanikiwa kufunga mabao manne na kutoa pasi saidizi mbili ndani ya msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC.
Maxi Nzengeli Young Africans,nae hayuko mbali msimu huu kwani kiungo huyo amefunga mabao matatu na kutoa pasi saidizi tatu hivyo kuhusika katika mabao sita.
Takwimu hizi zinaonesha ushindani mkubwa wa wachezaji katika kuchangia mafanikio ya timu zao, huku Gueye akionekana kuwa na mwanzo mzuri katika mbio za kuwania nafasi ya mchezaji mwenye mchango mkubwa zaidi katika mabao msimu huu