Uwezo wa kutumia vyema mipira iliyokufa (Set Pieces) unaendelea kuwa moja ya silaha muhimu kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027, huku Simba SC ikionyesha ubora zaidi katika eneo hilo kwa kuongoza orodha ya timu zilizofunga mabao mengi kupitia mipira iliyokufa.
Kwa mujibu wa takwimu za Ligi Kuu ya NBC, timu ya Simbai naongoza ikiwa imefunga mabao nane, ikionyesha namna ambavyo timu hiyo imekuwa na uwezo wa kutumia vyema mipira ya kona, faulo na mipira mingine iliyosimama kupata mabao.
Polisi Tanzania inashika nafasi ya pili ikiwa na mabao sita, ikiendelea kuonyesha kuwa mipira iliyokufa ni sehemu muhimu ya mfumo wao wa ushambuliaji.
Coastal Union na Pamba Jiji zinashika nafasi ya tatu na nne kila moja ikiwa imefunga mabao manne kupitia mipira iliyokufa, huku timu za Azam , Geita Gold na Young Africans zikikamilisha orodha hiyo kwa kufunga mabao matatu kila moja.
Takwimu hizi zinaonyesha umuhimu wa maandalizi maalumu ya mipira iliyokufa katika soka la kisasa, ambapo timu zinaweza kupata matokeo kupitia mikakati ya kona na faulo hata pale zinapokutana na ushindani mkali ndani ya mchezo hivyo kusaidia timu hizo kupata mabao yanayoweza kuzipatia timu hizo matokeo mazuri.