GEITA YAPATA ALAMA TATU ‘JIONI’, KAGERA, TRA WAGAWANA ALAMA.

MZUNGUKO wa 12 wa Ligi Kuu ya NBC umetamatika kwa michezo miwili ambapo Kagera Sugar ilicheza na TRA United huku Geita Gold ikiikaribisha timu ya Mashujaa.

Mchezo wa kwanza ulichezwa uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera majira ya saa 12:30 jioni ambapo mchezo ulikuwa muhimu kwa timu zote ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupambania ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

Iliwachukua dakika 42 timu ya Kagera Sugar kufungua ukurasa wa mabao kupitia mchezaji wake Yassin Salehe hivyo hadi mapumziko matokeo yalikuwa 1-0.

Kipindi cha pili kilirejea TRA ikisaka bao la kusawazisha ambapo mbinu zao zilifanikiwa dakika ya 57 kupitia mchezaji Amy Mapaka na matokeo yalibaki 1-1 mpaka mwisho wa mchezo huo na Kiungo wa Kagera Sugar Yassin Salehe alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Mchezo wa pili ulichezwa uwanja wa Bukombe mkoani Geita ambapo Geita Gold iliikaribisha timu ya Mashujaa mchezo uliochezwa saa 2:30 usiku.

Ulikuwa mchezo muhimu kwa timu zote ili kuiimarisha kutoka nafasi walizopo kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Mashujaa ndio ilikuwa timu ya kwanza kufungua ukurasa wa mabao kupitia mchezaji wake Mudathir Vuai dakika ya 43 ya mchezo huo na dakika tatu baadae mshambuliaji wa Geita Gold Fabrice Ngoy alisawazisha hivyo mzani kuwa sawa hadi wakati wa mapumziko matokeo yalikuwa 1-1.

Kipindi cha pili kilirejea kila timu ikihakikisha inapambana kuweza kupata matokeo ambapo Geita Gold ilifanikiwa dakika ya 88 baada ya mchezaji wao Arnaud Noah kuipatia bao la pili timu hiyo hivyo dakika 90 zilitamatika kwa matokeo ya 2-1 na mchezaji wa Geita Gold Arnaud Noah alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *