TIMU ya Simba imeendelea kushika rekodi ya kutokufungwa mchezo wowote ndani ya Ligi Kuu ya NBC baada ya kucheza michezo 11 ndani ya msimu wa 2026/2027 wa Ligi hiyo bila kufungwa wala kutoa sare.
Timu hiyo inashika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na alama 33 ikifunga mabao 25 na kufungwa mabao 7.
Young Africans ndio wanafuata kwenye msimamo huo wakiwa na alama 28, ushindi michezo tisa, sare moja na kufungwa mchezo mmoja aidha timu hiyo imefunga mabao 25 ikiruhusu mabao matano.
Azam ipo nafasi ya tatu ikicheza michezo 11 ushindi saba, sare mbili na kupoteza michezo miwili pia timu hiyo imefunga mabao 21 ikiruhusu mabao 12 huku ikikusanya alama 23.
Singida Black Stars ipo nafasi ya nne ikiwa imekusanya alama 17 baada ya kushinda michezo mitano sare mbili na kufungwa michezo minne huku ikifunga mabao 19 na kufungwa mabao 14.
Dodoma Jiji imevuna alama 17 baada ya kushinda michezo minne sare tano na kupoteza michezo miwili aidha timu hiyo imefunga mabao nane na kufungwa mabao matano
JKT Tanzania ipo nafasi ya sita imevuna alama 16 baada ya kushinda michezo mitano sare moja na kupoteza michezo sita aidha timu hiyo imefunga mabao 12 na kufungwa mabao 15.
Namungo haipo mbali nayo imevuna alama 17 baada ya kushinda michezo minne sare tano na kupoteza michezo miwili aidha timu hiyo imefunga mabao nane na kufungwa mabao matano
Polisi Tanzania imevuna alama 15 baada ya kushinda michezo minne sare tatu na kupoteza michezo mitano, timu hiyo imefunga mabao 13 na kufungwa mabao 14.
Mashujaa imevuna alama 15 baada ya kushinda michezo mitano na kupoteza michezo sita aidha timu hiyo imefunga mabao 12 na kufungwa mabao 17 huku ikiwa nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Mbeya City imevuna alama 14 baada ya kushinda michezo minne sare mbili na kupoteza michezo minne aidha timu hiyo imefunga mabao 9 na kufungwa mabao 13 huku ikiwa nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Coastal Union imevuna alama 14 baada ya kushinda michezo minne sare mbili na kupoteza michezo sita aidha timu hiyo imefunga mabao 11 na kufungwa mabao 16 huku ikiwa nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
TRA United imevuna alama 12 baada ya kushinda michezo miwili, sare sita na kupoteza michezo mitatu, timu hiyo imefunga mabao 11 na kufungwa mabao 11 huku ikiwa nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Geita Gold imevuna alama 12 baada ya kushinda michezo mitatu , sare tatu na kupoteza michezo sita aidha timu hiyo imefunga mabao 13 na kufungwa mabao 16 huku ikiwa nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Pamba Jiji imevuna alama tisa baada ya kushinda michezo miwili, sare tatu na kupoteza michezo saba, timu hiyo imefunga mabao 13 na kufungwa mabao 19 huku ikiwa nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Fountain Gate imevuna alama saba baada ya kushinda mchezo mmoja, sare nne na kupoteza michezo saba aidha timu hiyo imefunga mabao saba na kufungwa mabao 17 huku ikiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kagera Sugar ipo nafasi ya Mwisho kwenye msimamo ikiwa imecheza michezo 12 ushindi mchezo mmoja sare nne kufungwa michezo saba huku ikifunga mabao 10 na kuruhusu mabao 23 huku ikivuna alama saba.