SHALULILE, JABIRI HAPATOSHI UFUNGAJI BORA.

VITA ya kiatu cha ufungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC imezidi kukolea kutokana na namna washambuliaji Peter Shalulile na Anuary Jabir wanavyokimbizana kwenye namba za mabao.

Peter Shalulile ni mshambuliaji wa timu ya Young Africans amecheza dakika 707 ndani ya michezo 10 amefanikiwa kufunga mabao saba.

Anuary Jabir ni mshambuliaji wa timu ya Polisi Tanzania amefanikiwa kufunga mabao saba akitumia dakika 974 ndani ya michezo 12 ya Ligi Kuu ya NBC.

Jonathan Sowah ni mshambuliaji wa timu ya Singida Black Stars amefanikiwa kufunga mabao matano akitumia dakika 444 ndani ya michezo saba.

Elie Mpanzu ni kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba akicheza dakika 774 ndani ya michezo 11 na kufunga mabao matano

Herbet Lukindo wa Namungo amefunga mabao matano ndani ya Ligi Kuu ya NBC akitumia dakika 567 ndani ya michezo tisa.

Obrey Chirwa wa Geita Gold amefunga mabao matano akitumia dakika 780 ndani ya michezo 10 ya Ligi Kuu ya NBC

Maabad Maabad wa timu ya Coastal Union amefanikiwa kufunga mabao matano msimu huu akitumia dakika 877 ndani ya michezo 11 ya Ligi Kuu ya NBC .

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *