MBISA KINARA HATI SAFI.

UBORA wa Ligi Kuu ya NBC unachangiwa na uwepo wa magolikipa bora ili kuimarisha eneo la ulinzi wa timu akisaidiana na mabeki wa timu.
Hawa hapa makipa wenye hati safi nyingi msimu huu hadi sasa;

Musa Mbisa ni golikipa wa timu ya Dodoma Jiji akiwa amecheza dakika 688 za michezo nane msimu huu, amefanikiwa kuwa na hati safi sita.

Djigui Diarra wa Young Africans msimu huu amecheza dakika 900 ndani ya michezo 10 amefanikiwa kuondoka na hati safi sita.

Djibrilla Kassali ni golikipa wa timu ya Simba, ameondoka na hati safi tano akiwa amecheza dakika 804 ndani ya michezo tisa.

Golikipa wa Namungo Suleiman Abraham amecheza michezo 11 ikiwa ni sawa na dakika 990, amefanikiwa kubeba hati safi tano.

Christopher Nyakanda wa Polisi Tanzania amecheza michezo 11 sawa na dakika 990 zilimtosha kuondoka na hati safi nne.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *