HAWAJAFUNGWA NYUMBANI HADI SASA KWENYE LIGI YA CHAMPIONSHIP YA NBC.

TIMU saba za Ligi ya Championship ya NBC zimeendeleza ubabe ndani ya ligi hiyo baada ya kutokubali kuruhusu kichapo katika viwanja vyao vya nyumbani msimu huu wa 2026/2027.

Mtibwa Sugar ni kinara wa Ligi hiyo imecheza michezo sita katika uwanja wao wa Manungu ikafanikiwa kushinda michezo mitano na sare moja.

Tanzania Prisons uwanja wao wa nyumbani ni Sokoine mkoani Mbeya ikiwa nafasi ya pili imecheza michezo mitano nyumbani na imeshinda michezo yote.

KMC uwanja wa nyumbani kwao ni KMC Complex uliopo Dar es Salaam imecheza michezo sita ikishinda michezo mitatu na sare michezo mitatu.

Bandari Tanzania ya Mtwara inatumia uwanja wa Nangwanda Sijaona imecheza michezo mitano nyumbani ushindi tatu na sare mbili.

Rhino Rangers ya Tabora imecheza michezo minne katika uwanja wake wa nyumbani wa Ali Hassan Mwinyi ikishinda mchezo mmoja na sare moja.

IAA ya Arusha imecheza michezo yake ya nyumbani katika uwanja wa Agakhan Arusha ikishinda michezo miwili na sare mbili.
Stand United uwanja wake ni Kambarage mkoani Shinyanga imecheza michezo sita ikishinda michezo mitatu na sare tatu.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *