HAMDANI ATIKISA LIGI YA CHAMPIONSHIP YA NBC.

 

Mshambuliaji Hamdani Ally wa Transit Camp ameendelea kung’ara katika Ligi ya championship msimu wa 2026/27 akiongoza orodha ya wafungaji baada ya kufunga mabao 12 huku akiwazidi washindani wake kwa tofauti ya mabao matatu.

Hamdani amekuwa na mwanzo mzuri wa msimu akionyesha uwezo mkubwa wa kutumia nafasi anazozipata na kuwa tishio kwa safu za ulinzi za wapinzani hali inayomuweka kileleni hadi sasa.

Katika nafasi ya pili Ramadhani Kalanje wa KMC anaendelea kumfuatilia kinara huyo akiwa amefunga mabao tisa idadi sawa na Abdulkarim Segeja wa Kigamboni United na Oscar Paulo
wa Tanzania Prisons ambao wamekusanya mabao tisa kila mmoja.

Nafasi ya Tano inashikiliwa na Abiudy Mtambuka mwenye mabao sita akiendelea kuwa miongoni mwa wachezaji wanaofuatilia kwa karibu ushindani wa wafungaji bora wa msimu huu.

Msimu huu wa 2026/27 bado unaendelea hivyo macho ya mashabiki yataendelea kuwa kwa washambuliaji hao katika safari ya kuwania tuzo ya ufungaji bora wa ligi Championship.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *