JUMLA ya mizunguko 17 sawa na michezo 136 ya Ligi ya NBC Championship tayari imeshachezwa na kushuhudia jumla ya mabao 302 yakifungwa mpaka sasa.
KenGold, Pamba, Mbeya kwanza na TMA ndiyo timu pekee ambazo hazijapoteza mchezo wowote wa nyumbani ndani ya Ligi ya NBC Championship mpaka kufikia hivi sasa.
Pamba,Mbeya Kwanza na TMA zimecheza michezo nane katika viwanja vyao vya nyumbani bila kufungwa huku KenGold ikicheza michezo saba pekee bila kufungwa.
Ruvu Shooting ndiyo timu iliyopoteza michezo mingi zaidi nyumbani baada ya kufungwa jumla ya michezo nane kwenye michezo 10 iliyocheza ndani ya uwanja wake wa nyumbani.