JUMLA ya mabao 13 yamefungwa kwenye michezo mitano (5) ya Ligi ya Championship ya NBC iliyochezwa leo Februari 26, 2025 kwenye mikoa minne tofauti.
Mtibwa Sugar ikiwa nyumbani kwake Manungu mkoani Morogoro imeibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Geita Gold mpinzani wake wa karibu kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC, kwa matokeo hayo Mtibwa inasalia kileleni mwa msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC ikifikisha alama 51 kwenye michezo 21 iliyocheza.
Transit Camp ikiwa nyumbani ikakubali kichapo cha bao 0-1 dhidi ya Green Warriors, Cosmopolitan ikapokea kichapo cha bao 0-1 dhidi ya Kiluvya huku Bigman ikiifunga Biashara UTD kwa bao 2-0.
Mchezo wa Mwisho kwa leo ulizikutanisha Mbuni dhidi ya Mbeya City ambapo Mbeya City ikiwa ugenini ikaibuka na ushindi wa mabao 1-3, ushindi huu unaipandisha Mbeya City hadi nafasi ya tatu (3) kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho Februari 27 kwa michezo miwili (2) kuchezwa ambapo African Sports itakuwa mwenyeji wa Polisi Tanzania huku TMA ikiwakaribisha Songea United.