ZIMESALIA siku tano (5) pekee kuelekea mchezo wa ‘DERBY’ ya Kariakoo ambapo Young Africans itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi ya Machi 8, 2025.
Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa timu iliyofunga mabao mengi zaidi kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu huu ikifunga (58) kwenye michezo 22 iliyocheza huku ikiruhusu mabao tisa pekee.
Kwa upande wa Simba silaha yao muhimu mpaka sasa ni kuzuia mabao ambapo kwa msimu huu ndio timu iliyoruhusu mabao machache zaidi ikifungwa mabao nane pekee kwenye michezo 21 iliyocheza mpaka sasa huku ikifunga mabao 46.
Yanga ipo kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 58 kwenye michezo 22 huku Simba ikiwa nafasi ya pili na alama 54 kwenye michezo 21 ikiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Dodoma Jiji utakaopangiwa tarehe mpya baada ya kuahirishwa kutokana na ajali iliyopata timu ya Dodoma mkoani Lindi.
Emanuel