JUMLA ya Michezo 136 kati ya 240 imeshachezwa kwenye Ligi ya Championship ya NBC msimu wa 2024/2025 na kushuhudia jumla ya mabao 297 yakifungwa kwenye michezo hiyo huku Mtibwa Sugar ikiwa kinara kwa kufunga mabao mengi.
Mtibwa imefunga jumla ya mabao 31 kwenye michezo 17 mengi zaidi kuliko timu yeyote kwenye Ligi ya Championship ya NBC hadi sasa huku ikiruhusu kufungwa mabao saba pekee machache zaidi kuliko timu yeyote kwenye Ligi hiyo.
Mtibwa inaongoza msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC ikiwa na alama 44 baada ya michezo 17 ikishinda michezo 14 ikipata sare michezo miwili na kufungwa mchezo mmoja pekee.
 
					