Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari 21, 2025 ilipitia mwenendo na matukio ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;
Ligi Kuu ya NBC
Mechi Namba 140: Mashujaa FC 0-0 Coastal Union
Klabu ya Mashujaa ya Kigoma imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi kinyume namatakwa ya Kanuni ya 17:21 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na kusababisha mdhamini mwenye haki yamatangazo ya runinga, Azam Media Limited kushindwakupata picha za tukio la timu kuwasili. Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi Namba 147: JKT Tanzania 0-1 Singida BS
Klabu ya Singida BS imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kutokutumia chumba maalumu cha kubadilishia nguo, kinyume na matakwa yaKanuni ya 17:20 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi Namba 150: Tabora United 1-1 KenGold
Klabu ya Tabora United imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la wawakilishi watimu hiyo kufika kwenye kikao cha maandilizi ya mchezo bila kifaa chochote kinyume na matakwa ya kanuni ya17:2(2.2) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 17:(2.2 & 62) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi Namba 151: Azam FC 2-0 Mashujaa FC
Klabu ya Mashujaa ya imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kuchelewakurejea kiwanjani baada ya muda wa mapumziko kumalizika. Mashujaa walichelewa kutoka vyumbani kwa dakika tano (5) jambo lililosababisha kuchelewa kuanzakwa kipindi cha pili.Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 17:(33 & 62) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mchezaji Seif Karihe wa Mashujaa ameadhibiwa kwa kufungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Azam FC, Feisal Salum. Karihe alimkanyaga Feisal wakati akiwa chini baada ya kumfanyia rafu.Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 41:5 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.
Mechi Namba 155: Namungo FC 0-3 Simba SC
Mchezaji wa Namungo Daniel Amoah ameadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kuonekana akimwaga vimiminika kwenye goli jambolililohusianishwa na vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina.Amoah alionekana akifanya tukio hilo wakati timu ya Simba ikijiandaa kupiga penati.Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 41:3 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.
TAARIFA
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imefuta adhabuya kadi nyekundu kwa mchezaji wa Namungo, Derick Mukombozi aliyoadhibiwa na mwamuzi wa mchezo tajwahapo juu. Kamati imefikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kuwa maelezo yyaliyopo kwenye ripoti yamwamuzi hayana ushahidi wa kutosha unaoendana namarejeo ya picha mjongeo.
Mechi Namba 157: Mashujaa 2-0 Pamba
Klabu ya Mashujaa ya mkoani Kigoma imeadhibiwa kwakupewa onyo kali kwa kosa la Watoto waokota mipira (ball kids) kuchelewa kwa makusudi kurejesha mipira uwanjanikwa wakati. Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 17:48 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za mchezo.
Mchezaji wa klabu ya Pamba Jiji ya Mwanza, KassimSuleiman ameadhibiwa kwa kufungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kumpiga kwa kutumia mpira ‘Ball Kid’ baada ya kukaa nampira huo muda mrefu bila kuurejesha kiwanjani. Mchezaji huyo aliadhibiwa kwa kadi nyekundu pia na mwamuzi wa mchezo kwa kosa hilo Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 41:5 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.
Mechi Namba 159: Young Africans 2-1 Singida BS
Klabu ya Young Africans imeadhibiwa kwa kupewa onyo kali kwa kosa la viongozi wake kuingia kwenye eneo la kuchezea (pitch area) baada ya mchezo tajwa hapo juukukamilika.
Viongozi hao wa klabu ya Yanga walioingia uwanjani walisababisha kukosekana kwa utulivu wakati wamahojiano ya mdhamini mwenye haki za matangazo yaruninga.Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 17:50 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi Namba 160: KenGold 1-0 Kagera Sugar
Klabu ya KenGold imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la maafisa wake kuchelewa kuwasili kwenye kikao cha maandalizi ya mchezo (MCM). Maafisa hao walifika kwenye kikao saa 4:30asubuhi badala ya saa 4:00 asubuhi kinyume na matakwaya Kanuni ya 17:2(2.2) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Ligi ya Championship ya NBC
Mechi Namba 151: Stand United 2-1 TMA
Klabu ya TMA imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kuharibu uzio wauwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga. TMA walifanya uharibifu huo ili wachezaji wao wapite chini ya uzio badala ya kupita kwenye mlango rasmi.
TMA walitumia eneo hilo la uzio lililoharibiwa kwa kuingiakiwanjani wakati wa kupasha misuli moto, wakati wakwenda kuanza kwa mchezo, wakati wa mapumziko nabaada ya mchezo kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:21 ya Ligi ya Championship kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 17:62 ya Ligi yaChampionship kuhusu Taratibu za Mchezo.