UTAMU wa Ligi Kuu ya NBC unazidi kukolea ikiwa ni mzunguko wa 27 wa Ligi hiyo huku timu ya Young Africans ikiongoza kwa kufunga mabao mengi ndani ya eneo la boksi (18).
Young Africans imefanikiwa kufunga mabao 55 ndani ya boksi ikiwa ni mabao mengi kufungwa na timu kwenye Ligi Kuu ya NBC.
Simba nayo haina mzaha ikiwa ndani ya boksi ambapo hadi sasa ikifanikiwa kufunga mabao 48 huku Azam ikiwa na mabao 38 kwenye eneo hilo la 18.
Singida Black Stars nayo haina utani iwapo wachezaji wake wakipata mpira ndani ya boksi ikiwa imeshafunga mabao 37 huku Tabora United na Dodoma Jiji zikiwa na mabao 23.
Kwa upande wa Namungo imefanikiwa kufunga mabao 22 na Fountain Gate ikifunga mabao 20 ndani ya eneo hilo la 18.