Baada ya kuchezwa kwa mizunguko 18 ya Ligi ya Championship ya NBC, jumla ya mabao 325 yamefungwa katika michezo 140 iliyochezwa hadi sasa, hali inayoonesha ushindani mkubwa miongoni mwa timu shiriki.
Mbeya Kwanza wanaongoza kwa ufungaji wa mabao, wakiwa wamefumania nyavu mara 37 huku wakiruhusu mabao 18. Kagera Sugar wanafuatia kwa karibu, wakiwa wamefunga mabao 33 na kuruhusu mabao 10 pekee, wakionesha uimara mkubwa katika safu ya ulinzi.
Vinara wa ligi hiyo kwa sasa, Geita Gold, wana uwiano bora wa mabao (goal difference), Timu hiyo imefunga mabao 32 na kuruhusu mabao nane tu, hivyo kuwa na tofauti ya mabao 24 takwimu inayodhihirisha uimara wao katika ushambuliaji na ulinzi.
Kwa upande mwingine, Barberian wanaoshika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC, ndio timu yenye idadi ndogo zaidi ya mabao ya kufunga, wakiwa wamefunga mabao 10 pekee na kuruhusu mabao 29.
‘Wana Kimanumanu’ African Sports ndio timu iliyoruhusu mabao mengi zaidi hadi sasa, wakiwa wamefungwa mabao 33 katika michezo 18 waliyocheza, huku wao wakifanikiwa kufunga mabao 14.
Can I get chance to show my talent play in club for future goals of club , I can perform CB,CDM,CM and CAM position , football is my passion and I’ll play with all heart to archive club objectives