LIGI KUU YA NBC HAKUNA ‘KUPOA’.

MZUNGUKO wa 27 wa Ligi Kuu ya NBC utaanza leo katika uwanja wa KMC Complex Dar es Salaam huku KMC na Coastal Union zikitarajia kufungua pazia la mzunguko huo saa 10:00 alasiri.

KMC ambayo tayari imeaga Ligi Kuu ya NBC baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya TRA itakuwa na ‘kibarua’ cha kuwapa furaha mashabiki wake mbele ya Coastal inayopambana kusalia kwenye Ligi msimu ujao.

Kesho juni 16 michezo itakuwa miwili ambapo Namungo itakuwa mwenyeji wa TRA United majira ya saa kumi katika uwanja wa Majaliwa Lindi huku Azam ikivaana na Mashujaa saa moja usiku.

Juni 17 Mbeya City itaikaribisha timu ya Simba majira ya saa nane mchana kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya huku vita ya kanda ya kati ikizikutanisha Singida Black Stars ya Singida na Dodoma Jiji ya Dodoma saa 10:00 alasiri katika uwanja wa Airtel Singida.

Michezo mitatu ya mwisho itakuwa juni 18 majira ya saa kumi jioni ambapo Fountain Gate itaialika Young Africans katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha huku mchezo wa Pamba Jiji dhidi ya Mtibwa ukipigwa CCM Kirumba jijini Mwanza na ‘maafande’ wa JKT Tanzania dhidi ya Tanzania Prisons wakifunga mzunguko katika uwanja wa Meja Jen Isamuhyo Dar es Salaam.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *