VITA ya pasi za mabao imezidi kushika kasi kutokana na namna wachezaji mbalimbali wanavyopambana kuhakikisha wanazidi kusaidia timu zao kupata alama za Ligi Kuu ya NBC.
Kiungo Elie Mpanzu wa Simba ndio kinara wa kutoa pasi za mwisho amefanikiwa kucheza dakika 1187 ndani ya michezo 21 ya Ligi Kuu ya NBC akitoa pasi za mabao nane mpaka sasa akiwa sawa na Feisal Salum wa Azam mwenye idadi hiyo ya pasi akiwa amecheza michezo 25 ya Ligi Kuu ya NBC akitumia dakika 2005 .
Allan Okello wa Young Africans ambaye aliingia kwenye Ligi Kuu ya NBC katika dirisha dogo la usajili amecheza micheza 20 ambayo ni sawa na dakika 1452 akiwa amefanikiwa kutoa pasi za mabao saba hadi sasa.
Sambamba na Okello yupo Iddi Selemani wa Azam mwenye idadi hiyo ya pasi baada ya kucheza dakika 1608 sawa na michezo 21 ya Ligi Kuu ya NBC.
Kiungo wa Simba raia wa Zambia Clatous Chama hayuko mbali akicheza dakika 2014 sawa na michezo 26 na kufanikiwa kutoa pasi sita za mabao.
Duke Abuya wa Young Africans amecheza dakika 2096 sawa nanichezo 25 akifanikiwa kutoa pasi za mabao sita .
Kwa upande wa Maxi Nzegeli wa Young Africans mpaka sasa ameshacheza dakika 2169 sawa na michezo 26 ya Ligi Kuu ya NBC akiwa na pasi sita pia.