MPANZU AIBEBA SIMBA,NDUMUMWE AKIWEKA REKODI MPYA LIGI KUU YA NBC.

Timu ya Simba imeendelea kuweka presha katika mbio za Ligi Kuu ya NBC baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Mbeya City katika mchezo uliochezwa jana mkoani Mbeya kwenye uwanja wa sokoine.

Bao pekee la mchezo lilifungwa na Elie Mpanzu dakika ya 43, akimalizia vyema shambulizi la Simba na kuwapa ‘Wekundu wa Msimbazi’ uongozi ambao waliulinda hadi filimbi ya mwisho.

Ushindi huo unaifanya Simba kuendelea kukusanya alama muhimu katika hatua za mwisho za msimu ikikusanya alama 64 na kukaa nafasi ya kwanza ikiwa mchezo mmoja mbele ya timu inayofuata ya Young Africans.

Mchezaji Bora wa mchezo Elie Mpanzu Simba alifunga bao la ushindi lililoamua matokeo ya mchezo na kuonyesha kiwango bora katika eneo la ushambuliaji na akiongoza Simba kupata alama zote tatu.

Katika mchezo mwingine uliokuwa ukichezwa mkoani Singida uwanja wa Airtel ambao Singida Black Stars iliibuka na ushindi mkubwa wa mabao 5-0 dhidi ya Dodoma Jiji .

Nyota wa mchezo huo alikuwa Ndumumwe Mossi, aliyefunga mabao matatu (hat-trick) akiiongoza Singida Black Stars kupata ushindi mnono mbele ya mashabiki wao.

Mabao mengine yalifungwa na Linda Mtange dakika ya 40 na Mishamo Daudi dakika ya 67 huku Singida Black Stars ikitawala mchezo kuanzia mwanzo hadi mwisho kwa kuonyesha ubora mkubwa katika umiliki wa mpira, utengenezaji wa nafasi na umaliziaji makini, huku safu yao ya ulinzi ikihakikisha Dodoma Jiji haipati nafasi ya kutikisa nyavu.

Ndumumwe Mossi aliyeonyesha kiwango bora aliibuka mchezaji bora wa mchezo akiichangia ushindi kwa kufunga mabao matatu (hat-trick) na kuwa nyota wa mchezo.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *