Mabingwa wa makundi ya Ligi ya First League kutoka kundi A na B msimu wa 2025/26, Rhino Rangers waliokuwa kundi B na Bandari Tanzania walikuwa kundi A , leo Juni 17, 2026, watashuka dimbani katika mchezo wa fainali wa kumtafuta bingwa wa jumla wa Ligi ya First League.
Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku, huku ukiwa na uzito mkubwa kwa timu zote mbili ambazo tayari zimefanikiwa kupanda daraja kwenda Ligi ya Championship ya NBC kwa msimu wa 2026/27 baada ya kutwaa ubingwa wa makundi yao.
Mbali na kuwania taji la bingwa wa jumla wa First League mechi hiyo itakuwa ya heshima na kujivunia mafanikio ya msimu mzima ambapo mshindi atamaliza kampeni akiwa ndiye bingwa rasmi wa First League 2025/26.
Mashabiki wa soka wanatarajiwa kushuhudia pambano kali kati ya timu mbili zilizoonyesha ubora na uthabiti katika safari yao ya kupanda daraja ambapo Mchezo huo utarushwa mubashara kupitia Azam Sports 1 HD, huku sherehe za kukabidhi kombe la ubingwa zikifanyika mara baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa.